FAHAMU MTI UNAOTIBU MAGONJWA MENGI - MLONGE
Moringa (Moringa spp.)
maarufu kama Mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu
ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na
hutumika kama chakula cha
binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji.
Faida na matumizi ya mti wa Moringa
Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti
wa Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote
ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi
mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi. Pia majani yanaweza
kutumika kama lishe bora ya mifugo.
Utafiti wa kisayansi
umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana.
Virutubishi hivi ni pamoja na;
Vitamini C -
Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa
mbalimbali. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni zaidi ya mara saba ya ile
inayopatikana kutoka kwenye machungwa.
Calcium (madini
chuma)- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa
na meno mwilini. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya
yale yanayopatikana kutoka kwenye maziwa.
Protini-
Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango
chake katika majani ya Moringa ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka
kwenye maziwa.
Vitamini A-
Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona.
Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana
kutoka kwenye Karoti.
Potassium-
Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango
chake katika majani ya Moringa ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka
kwenye ndizi.
Maua ya Moringa yamejaliwa
madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa
na kuliwa kama mboga.
2. Mboga
Majani ya Moringa
huliwa kama mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa
wakati wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani.
Pia matunda mateke ya
Moringa huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi
(machanga).
Matunda yalikomaa hutoa
mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.
3. Mafuta
Mafuta kutoka kwenye mbegu
za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia
hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo.
Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.
4. Lishe ya Mifugo
Majani ya Moringa
huliwa na ng’ombe, mbuzi, kondoo, sungura na kuku. Mbegu huliwa na kuku pamoja
na wanyama wengine kwenye jamii ya ndege.
5. Pambo la nyumba
Mti wa Moringa hupandwa
kwa wingi kwenye bustani kama ua au mti wa kivuli na hutumika katika upambaji.
Pia miti ya moringa ikipandwa karibu karibu inaweza kutumika kama fensi.
6. Chanzo cha kipato
Mti wa Moringa
ukitumiwa vizuri ni chanzo kizuri cha kipato. Mfano ni uuzaji wa miche ya mti
wa moringa na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na moringa.
7. Tiba mbadala
Moringa ni mti muhimu
sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake
hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali.
Majani
• Majani mabichi ya
Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi
wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
• Juisi ya majani ya
Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi
ikichanganywa na asali inatibu kuharisha.
• Pia juisi ina uwezo
wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye
kisukari.
• Majani pia huweza
kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.
Mbegu
• Mbegu za mti wa
Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri
ngozi.
• Pia mbegu hutuminka
katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye
tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha
maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.
Magome
• Magome ya mti wa
Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili
kupunguza maumivu yatokanayo na kung’atwa na wadudu kama nyoka na nge.
Matumizi mengineyo
Miti ya Moringa
ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandayo kama vile maharage.
Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la moja kwa moja
kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano wa mboga kusinyaa au
kukauka.
Namna ya kupanda mti wa
Moringa
Mti wa Moringa unaota
katika mazingira yote, kwenye ukame na meneo yenye maji. Angalizo huchukuliwa
kuhakikisha kuwa maji hayatuami kwenye mti kwasababu maji huweza kusababisha
ugonjwa na kufanya mizizi ioze. Karibu aina zote za udongo zinafaa kwa mti wa
Moringa. Mbegu, kipande cha tawi na hata mzizi vinaweza kutumika koutesha mti
wa moringa.
I. Mbegu
Mbegu iliyokomaa ya mti
wa Moringa hulowekwa siku moja kabla ya kuoteshwa, kama maji sio tatizo mbegu
inaweza kupandwa moja kwa moja kwenye udongo baada ya kuchimba shimo, weka maji
na kisha changanya udongo na samadi angalau kilo tano kabla ya kupanda mbegu
halafu endelea kumwagilia katika miezi ya mwanzo. Baada ya angalau siku kumi na
tano mbegu inatakiwa iwe imeshachipua.
Pia unaweza kuotesha
mbegu za Moringa katika vifuko kwenye kitalu kisha kuhamishia shambani baada ya
kuota.
II. Kipande cha tawi
Vipande vya tawi lililo
komaa huweza kutumika katika kupanda mti wa Moringa, hivi hupandwa eidha moja
kwa moja shambani au kwenye vifuko katika kitalu. Kama ukipandwa moja kwa moja
angalau robo moja ya tawi inatakiwa ipandwe kwenye udongo, usimwagilie maji
mengi sana kwani inaweza kusababisha kuoza
0 Comments